1 John 2:1-6

Al-Masihi Mwombezi Wetu

1 aWatoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Isa Al-Masihi, Mwenye Haki. 2 bYeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.

3 cBasi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 4 dMtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 5 eLakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. 6 fYeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Isa alivyoenenda.

Amri Mpya

Copyright information for SwhKC